• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia yasema ukuaji wa uchumi wa eneo la Afrika kusini mwa Sahara kwa mwaka huu utapungua kwa asilimia 2.8

    (GMT+08:00) 2020-06-10 09:41:14

    Benki ya Dunia imetoa ripoti ikisema, kutokana na athari ya janga la COVID-19 ukuaji wa uchumi wa eneo la Afrika kusini mwa Sahara kwa mwaka huu unakadiriwa kupungua kwa asilimia 2.8.

    Ripoti ya Matarajio ya Uchumi wa Dunia iliyotolewa na Benki ya Dunia imesema, thamani ya jumla ya uzalishaji kwa mtu barani Afrika pia itapungua kwa kasi, na mamilioni ya watu wataangukia kwenye ufukara.

    Ripoti hiyo imesema kama janga la COVID-19 likipungua katika nusu ya pili ya mwaka huu, ukuaji wa uchumi utaweza kufikia asilimia 3.1 mnamo mwaka 2021.

    Ripoti pia imesema licha ya athari kubwa hasi ya janga la COVID-19 kwa usalama na afya, hatua za kukinga na kudhibiti COVID-19 ambazo ni pamoja na zuio la usafiri na ufungaji wa mipaka, pia zimeharibu uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako