• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wazitaka pande zinazopambana nchini Libya zifuate sheria ya kibinadamu ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2020-06-10 09:41:38

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amezitaka pande zinazopambana nchini Libya zifuate sheria ya kibinadamu ya kimataifa, hasa kuhakikisha usalama wa hospitali na shule, na kuwezesha utoaji wa misaada.

    Bw. Mahamat amesisitiza mwaliko wake wa tarehe 27 mwezi Machi kwa pande hasimu nchini Libya kuhusu kusitisha mapambano mara moja na kufanya mazungumzo chini ya utaratibu wa Taarifa ya Berlin. Amesema Umoja wa Afrika uko tayari kusaidia kutekeleza makubaliano ya usitishaji wa mapambano, na kutoa mchango kwa ajili ya kuweka mazingira ya lazima kwa wadau wa Libya kurudi kwenye mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako