• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Bingwa wa Cardiff Marathon awapa wanariadha walioathiriwa na COVID-19 nyumba zake kuishi bila malipo

    (GMT+08:00) 2020-06-10 16:22:28

    Bingwa wa zamani wa Cardiff Half Marathon raia wa Kenya, John Kipsang Lotiang, amewapa wanariadha ambao wameathiriwa zaidi na janga la corona nyumba saba za kukodisha bila malipo. Mwanariadha huyo mzawa wa Pokot Magharibi ametoa bure jumla ya nyumba saba za kienyeji na za kisasa alizozijenga katika eneo la Mororia, kilomita tatu kutoka mjini Iten. Nyumba hizo zilizokamilishwa kujengwa wiki mbili zilizopita, zitawapa hifadhi wakimbiaji ambao kwa sasa wana shida ya sehemu ya kuishi ama kulipa kodi wakati huu mgumu wa hali ya kiuchumi. Hata hivyo, hajafichua mfumo atakaotumia kuteua wanariadha watakaonufaika na msaada wake huo hasa ikizingatiwa kwamba zaidi ya kambi 140 za mazoezi ya wanariadha katika kaunti za Pokot, Uasin Gishu na Elgeyo-Marakwet zimefungwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako