• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CPI ya China yaongezeka kwa asilimia 2.4 mwezi Mei kuliko mwaka jana wakati kama huu

    (GMT+08:00) 2020-06-10 19:19:01

    Idara ya Takwimu ya China imeonesha kuwa, ongezeko la bei za bidhaa za matumizi kwa mwezi Mei nchini China CPI iliongezeka kwa asilimia 2.4 kuliko mwaka jana wakati kama huu, kiasi ambacho kimepungua kwa asilimia 0.8 kuliko mwezi uliopita. Wataalamu wameeleza kuwa, kupungua kwa bei ya chakula kunachangia zaidi kupungua kwa CPI kuliko mwezi uliopita.

    Takwimu zimeonesha kuwa, bei ya chakula kwa mwezi Mei iliongezeka kwa asilimia 10.6 kuliko mwaka jana wakati kama huu, ongezeko hilo limepungua kwa asilimia 4.2, huku bei ya bidhaa zisizo za chakula imeongezeka kwa asilimia 0.4, kiasi ambacho kinalingana na mwezi uliopita. Kati ya aina mbalimbali za chakula, bei ya nyama ya nguruwe imeongezeka kwa asilimia 81.7, ongezeko hili limepungua kwa asilimia 15.2 kuliko mwezi uliopita, wakati huo huo kiwango cha ongezeko la bei za nyama ya ng'ombe, mbuzi, kuku na bata pia kimepungua, bei za matunda, mayai na mboga pia zimepungua kwa kiasi kikubwa.

    Mtafiti wa Ofisi ya washauri waandamizi wa Baraza la Serikali la China Bw. Yao Jingyuan ameeleza kuwa, kupungua kwa bei za nyama ya nguruwe na mboga ni sababu kuu ya kushuka kwa CPI ikilinganishwa na mwezi Mei. Anasema:

    "Tokea mwaka jana, China ilichukua hatua mbalimbali kuweka mpango kwa njia ya kisayansi kuhusu ufugaji wa nguruwe. Mbali na hayo mwezi Mei kutokana na kurejeshwa kwa uzalishaji mali, na hali nzuri ya hewa imesaidia uzalishaji wa mboga, hali ambayo imechangia kushuka kwa CPI."

    Bw. Yao Jingyuan anaona kuwa, kushuka kwa ongezeko la CPI kuna umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya uchumi. Anasema:

    "Kinachowafurahisha watu ni kuwa, CPI ya China inaweza kubaki kwenye kiwango cha chini tena kwenye hali yenye utulivu, hali ambayo inaweka mazingira mazuri kwa ajili ya sera ya sarafu. Utulivu wa bei za bidhaa unaweka mazingira muhimu ya kimsingi kwa ajili ya China kutimiza malengo muhimu sita ."

    Bw. Yao pia ameeleza kuwa kupungua kwa ongezeko la CPI vilevile kumeonesha kuwa uzalishaji mali unarejeshwa hatua kwa hatua, na uchumi pia unazidi kufufuka. Anasema:

    "Hali hii inaonesha kurejeshwa kwa uzalishaji wa mali, ambayo pia ni dalili ya kufufuka kwa uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako