• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Safaricom yafunga maduka kunyunyiza dawa

    (GMT+08:00) 2020-06-10 20:32:45
    Kampuni ya huduma za mawasiliano nchini Kenya Safaricom imefunga maduka yake manne kwa muda wa siku mbili ili kuyanyunyuzia dawa kama hatua mojawapo ya kuepushia wafanyakazi na wateja hatari ya virusi vya corona.

    Maduka hayo ni lililo eneo la Nyali na lile la Rex House ambapo haya mawili ni ya mjini Mombasa, lile la Thika na lile la Lavington Mall yamefungwa hii leo Jumanne hadi Juni 11 watakapomaliza shughuli hiyo.

    Aidha kampuni hiyo imetangaza kwamba itakuwa ikiendeleza shughuli hiyo ya unyunyuziaji wa dawa mara kwa mara.

    Kwenye taarifa iliyochapishwa na Safaricom na kusambazwa kupitia akaunti yake ya Twitter kampuni hiyo ya mawasiliano imesema itakuwa inafanya shughuli hiyo mara kwa mara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako