• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Panga la kukatwa mshahara lawasubiri akina Molinga, Sibomana na Makame kwa kunenepa

    (GMT+08:00) 2020-06-11 08:53:35

    Nahodha msaidizi wa Klabu ya Yanga, Juma Abdul, amesema kuwa Kocha Mkuu, Luc Eymael aliwaambia wachezaji kwamba atakayeongezeka uzito atakatwa mshahara wake ikiwa ni sehemu ya adhabu. Abdul amesema kuwa Eymael aliwapa programu maalumu za kufanya kwa ajili ya kulinda vipaji vyao wakati wa mapumziko yaliyosababishwa na janga la Corona na kutoa onyo kwa wachezaji wote. Amesema anaamini kwamba Eymael atakapopewa ripoti kazi ya kwanza itakuwa ni kutazama wale ambao wameshindwa kutimiza vigezo vyake. Inaelezwa kuwa walioongezeka uzito ambao panga la mshahara linawasubiri ni pamoja na David Molinga, Patrick Sibomana na Abdulaziz Makame

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako