• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mauzo ya magari ya China yaongezeka kwa mwezi wa pili mfululizo

    (GMT+08:00) 2020-06-11 19:35:07
    Mauzo ya magari ya China yameongezeka kwa asilimia 14.5 mwezi Mei kutoka kipindi sawa na hicho mwaka jana.

    Takwimu zilizotolewa leo zinaonyesha kuwa soko kubwa la magari duniani limeanza kufufuka baada ya kuanguka kutokana na nchi kufungwa kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

    Matokeo hayo yalifuatia ongezeko la asilimia 4.4 mwezi Aprili na anguko la asilimia 43 mwezi Machi,wakati ambapo ugonjwa huo uliangusha mahitaji.

    Takwimu kutoka Chama cha Waundaji Magari cha China (CAAM) zinaonyesha kuwa mauzo katika mwezi Mei yaliongezeka hadi magari milioni 2.19.

    Afisa Mkuu wa CAAM,Chen Shihua,amesema msaada wa sera za serikali na uboreshaji wa ujasiri wa watumiaji zimechangia ukuaji katika mwezi Mei.

    Hata hivyo,Chen alisema ,maendeleo ya ugonjwa wa Corona huenda yakaathiri mahitaji ya magari ya China katika soko la kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako