• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Ighalo ashangazwa na mazoezi chini ya masharti mapya

    (GMT+08:00) 2020-06-12 17:13:14

    Mshambuliaji wa timu ya Manchester United Odion Ighalo amesema mazoezi anayofanya kwa sasa ni mapya kabisa katika maisha yake ya soka. United kama ilivyo timu zingine za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), ilirejea mazoezini kujiandaa kwa marejea ya michuano ya ligi hiyo, lakini chini ya vikwazo vikali vya afya. Ighalo anasema katika mazoezi ya sasa, ni lazima kukaa umbali wa mita mbili na mchezaji mwingine, na hata ukitaka kuongea ni lazima useme kwa sauti kubwa. Hata hivyo, nyota huyo amedai kwamba wachezaji wote wamefurahia mazoezi hayo kuliko walivyokuwa wakijinoa kivyao manyumbani mwao kutokana na janga la corona. Ighalo alieleza furaha yake kufuatia kurejea kwa Paul Pogba na Marcus Rashford, wakati timu hiyo inajiandaa kukutana na Tottenham Hotspur Juni 19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako