• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya jumla ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona barani Afrika yazidi laki 2.1

    (GMT+08:00) 2020-06-12 19:25:17

    Takwimu zilizotolewa na Kituo cha Kinga na Udhibti wa Magonjwa cha Afrika zimeonesha kuwa, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona barani Afrika imefikia 210,153, watu 5,692 wamefariki kutokana na virusi hivyo, na wengine 95,781 wamepona.

    Wakati huohuo, misaada iliyotolewa na China imefika katika nchi mbalimbali za Afrika kwa nyakati tofauti. Awamu ya tatu ya misaada ya afya ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona iliyotolewa na China kwa Sudan Kusini imewasili mjini Juba, ikiwa ni pamoja na mavazi ya kujikinga, barakoa na glavu.

    Hafla ya kukabidhi awamu ya pili ya misaada iliyotolewa na China kwa Zimbabwe pia imefanyika katika ikulu ya Zimbabwe.

    Mbali na hayo, misaada iliyotolewa na China juzi usiku pia imesafirishwa nchini Mauritania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako