• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kitendo cha Marekani cha kuipaka matope China kwa kuifanya Afrika ibebe madeni hakitafanya kazi

    (GMT+08:00) 2020-06-12 19:28:26

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chuanying leo hapa Beijing amesema, China na Afrika zimekuwa zikisaidiana na kushirikiana katika kupambana na virusi vya Corona, na China imetoa vifaa vingi vya kupambana na maambukizi ya virusi hivyo, na kupeleka wataalamu wa matibabu barani Afrika.

    Bi. Hua amesema hayo alipozungumzia ripoti kwamba, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo hivi karibuni ameeleza kuwa nchi hiyo imegundua kuwa China na kampuni zake binafsi zimetoa misaada kidogo, huku ikitoa mikopo isiyo wazi barani Afrika wakati wa mlipuko wa maambukizi ya virusi, na kwamba hatua hiyo imezifanya nchi za Afrika kubeba madeni makubwa.

    Hua Chunying amesisitiza kuwa, hivi sasa nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na maambukizi ya virusi hivyo, na anatumai pande zinazohusika zitafuatilia zaidi hatua za kuisaidia Afrika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako