• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shehena ya pili ya msaada wa China yakabidhiwa kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati

    (GMT+08:00) 2020-06-13 18:42:27

    Hafla ya kukabidhi shehena ya pili ya msaada wa vifaa vya matibabu dhidi ya COVID-19 iliyotolewa na serikali ya China kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati imefanyika kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Bangui.

    Rais Faustin Archange Touadera wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameishukuru China kwa kutoa msaada kwa watu wake wakati wanakabiliwa na wakati mgumu zaidi.

    Waziri wa ushirikiano wa uchumi wa nchi hiyo Bw. FĂ©lix Moloua amesema, tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona, China ikiwa rafiki wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, imetoa misaada mingi kwa nchi hiyo kuongeza uwezo wa kukabiliana na virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako