• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya maofisa wa ICC vyakosolewa

    (GMT+08:00) 2020-06-13 18:52:37

    Jumuiya ya kimataifa imekosoa vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya baadhi ya maofisa wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC wanaochunguza uwezekano kuwa wanajeshi wa Marekani walifanya uhalifu wa kivita nchini Afghanistan.

    Ikulu ya Marekani imesema Rais Donald Trump wa Marekani ameidhinisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya maofisa wa ICC "wanaohusika moja kwa moja na juhudi za kuchunguza na kuwachukulia hatua watumishi wa Marekani bila idhini ya Marekani, ikiwa ni pamoja na kupanua vizuizi vya kutoa visa kwa maofisa hao na wanafamilia wao.

    ICC imetoa taarifa ikisema Marekani kuishambulia mahakama hiyo "kuongeza changamoto na jaribio lisilokubalika la kuingilia utawala wa sheria na mwenendo wa kimahakama wa mahakama hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako