Soko kubwa la biashara ya jumla ya matunda, mbogambonga na nyama la Beijing Xinfadi, limefungwa kwa muda na kupuliziwa dawa baada ya watu wanaofanya kazi kwenye soko hilo na mazingira yake kugunduliwa kuwa na virusi vya Corona.
Msemaji wa kamati ya afya manispaa ya Beijing, amesema watu wote waliokaribia soko hilo tangu Mei 30 watafanyiwa upimaji. Amesema kwa sasa mji wa Beijing una vituo 98 vikiwa na uwezo wa kupima watu elfu 90 kwa siku.
Ijumaa Beijing ilitangaza watu sita wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona. Watu hao na mmoja aliyetangazwa kuambukizwa alhamisi wote wana uhusiano na soko la Xinfadi au watu wa karibu wana uhusiano na soko hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |