• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Acheni kuichochea Afrika dhidi ya China

    (GMT+08:00) 2020-06-14 19:10:23

    Hivi karibuni baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi wamechochea tena uhasama kati ya China na Afrika. Mwanahabari wa Vision Group Mubarak Mugabo ametoa makala yenye kichwa cha Acheni kuichochea Afrika dhidi ya China.

    Kwenye makala hiyo Mugabo amesema, katika miaka mingi iliyopita China imekuwa ikiwekeza pakubwa katika miradi ya miundombinu ya Afrika ikilenga kufungua soko la Afrika chini ya mpango wa ushirikiano kati ya China na Afrika. Kwa mfano nchini Uganda, serikali ya China imechangia majengo pacha ambayo yana ofisi za Rais na Waziri Mkuu, huku ikikarabati Ikulu ya Entebbe.

    Mbali na hapo serikali ya China pia imetoa zawadi ya kompyuta kwa takriban serikali za nchi 35, kukarabati majengo ya serikali, zikiwemo ofisi za marais, Mabunge, Makao makuu ya Umoja wa Afrika, ikulu na mengine mengi.

    Lakini kwa mujibu wa ripoti, haya yanaweza kutoa wepesi kwa Wachina kuzipeleleza serikali za Afrika na Marekani, makampuni na wanasiasa. Shutuma hizi zimekuja katika sakata la kulaumiana kati ya China na Marekani hasa katika wakati huu mgumu wa janga la Covid-19.

    Sasa inaonekana kwamba mapambano ya kiuchumi na kisiasa kati ya Marekani na China yamepoteza thamani yake katika mabara mengine ila kwa namna fulani yanafaa na yanahitajika katika bara la Afrika. Hata hivyo kuipeleleza Afrika ni kupoteza muda kwasababu bara hili halina nia mbaya hadi sasa ya kulishambulia bara jingine lolote lile kama waonyaji wanavyodai.

    Iweje China itake kutumia miradi kuipeleleza Afrika na sio Marekani ambao wana vituo vyao vya kijeshi zaidi ya 30 katika Afrika na karibu kila sehemu duniani. Marekani ina historia ya kupeleleza nchi za Afrika ili kujua kama serikali zina sera ambazo hazikidhi maslahi yao. Na mwisho wanadhamini upande wa upinzani ili kuziondoa serikali halali na zilizochaguliwa kidemokrasia na wananchi.

    Katika kipindi chote hicho China haijashawishika kudhamini au hata kupambana na serikali yoyote iliyowekwa madarakani kisheria katika Afrika.

    Swali la kujiuliza ni kwamba kwanini China iipeleleze Afrika? Kwa muda mrefu Afrika imekuwa ikinyimwa fursa ya sekta ya viwanda ili kusukuma mbele maendeleo yake ya uchumi kwasababu ya miundo mbinu yake dhaifu, lakini China imeliona hili na kuamua kulirekebisha na bado ipo ikiendelea kutoa usaidizi wake.

    Je China inapaswa kukabiliwa na mitazamo hasi inayotolewa juu yake? Hapana, kizazi kipya cha Afrika kinatakiwa kujua kwamba miundombinu inayotengenezwa katika Afrika ni kitu kinachohitajika kunufaisha kizazi cha sasa na vijavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako