• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika waisifu China kwa kutoa mchango muhimu katika mapambano dhidi ya COVID-19 barani Afrika

    (GMT+08:00) 2020-06-14 19:26:08

    Umoja wa Afrika jana uliishukuru China kwa kutoa mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya COVID-19 barani Afrika.

    shukrani hiyo ilitolewa kwenye taarifa ya mkutano kwa njia ya video wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika na wenyeviti wa Jumuiya ya uchumi ya Umoja wa Afrika.

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini aliongoza mkutano huo ambao ulilenga kupitisha ripoti za wajumbe maalumu wa Umoja wa Afrika kuhusu hatua za kusaidia uchumi na manunuzi ya vifaa tiba kwa nchi wanachama katika mapambano dhidi ya COVID-19.

    Wakuu hao walisifu mchango mkubwa uliotolewa na China, pamoja na kuisaidia Afrika kutimiza uwezo wa kutengeneza vitendanishi milioni 30, mashine za kupumulia 10,000 na barakoa milioni 80.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako