• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TANZIA: Katibu mkuu wa Chama cha mpira wa kikapu Tanzania Coach G afariki dunia

    (GMT+08:00) 2020-06-15 08:33:18

    Chama cha mpira wa kikapu kimethibitisha msiba wa katibu mkuu wake Yusuph Nyirenda, maarufu Coach G au Mzee G kilichotokea juzi katika Hospitali ya Wilaya Inyala majira ya saa mbili usiku alipokuwa akitibiwa baada ya kuugua kwa muda mfupi. Katika uhai wake atakumbukwa kwa kuendeleza mchezo wa kikapu mkoani Mbeya na Tanzania kwa ujumla. Atakumbukwa namna alivyowafunda wachezaji wengi na maarufu kuanzia miaka ya 80 mpaka umauti unamkumba kwenye Uwanja wa Mbeya Catholic youth centre, mafanikio ya mkoa wa Mbeya yamechangiwa nae kuanzia ligi mbali mbali mkoani, ushiriki wa ligi za Taifa na kimataifa, ubingwa wa Taifa mara tatu mfululizo. Atakumbukwa daima na wadau wa mpira wa kikapu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako