• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yasema kuchangia damu ni jambo muhimu katika kupambana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-15 09:30:33

    Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani WHO anayeshughulikia mambo ya Afrika Bibi Matshidiso Moeti, amesema nchi zote zinapaswa kuwekeza katika miundombinu na kampeni za kuongeza ufahamu wa umma, ili kuhimiza uchangiaji wa damu salama na kuimarisha mwitiko dhidi ya mlipuko wa COVID-19.

    Amesema kwenye kipindi maalumu cha janga la virusi vya Corona, utoaji wa damu salama unakabiliwa na changamoto, na shughuli za kuchangisha damu zimeahirishwa. Pia amesema kuvurugika kwa mnyororo wa ugavi duniani kunakotokana na COVID-19 kumetatanisha zaidi upungufu wa vifaa vinavyohitajika katika huduma ya kuchangia damu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako