• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanamgambo wa Al-shabab wamwua polisi wa akiba kaskazini mashariki mwa Kenya

    (GMT+08:00) 2020-06-15 09:53:23

    Kundi la Al-Shabab jana asubuhi limemwua polisi mmoja wa akiba wa Kenya katika mji wa Mandera, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

    Kamanda wa polisi wa eneo hilo Bw. Rono Bunei amesema mwanamgambo mmoja pia ameuawa wakati watu wenye silaha walipovamia mji huo baada ya kushindwa kuangusha mnara wa mawasiliano, na kukabiliwa na upinzani kutoka kwa vikosi vya usalama.

    Bw. Bunei amesema baada ya wanamgambo kushindwa kuangusha mnara wa mawasiliano, walimteka nyara polisi mmoja wa akiba, na mwili wake uligundiliwa umbali wa kilomita kadhaa.

    Habari nyingine zinasema jeshi la Somalia jumamosi limewaua wanamgambo 13 wa kundi la al-Shabab katika jimbo la kusini la Lower Juba.

    Kamanda wa kitengo cha 43 cha jeshi la taifa la Somalia SNA Bw. Ali Mohamed amesema jeshi hilo limefanya shambulizi baada ya kuarifiwa na umma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako