• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENNIS: Mashindano ya Wazi ya Tennis Marekani yatarajiwa kuanza licha ya wasiwasi wa wachezaji

    (GMT+08:00) 2020-06-15 15:35:31

    Hatma ya Mashindano ya Wazi ya Tennis Marekani (US Open) itajulikana baadaye wiki hii wakati maofisa watakapoamua kama mashindano hayo yataendelea kama ilivyopangwa licha ya kuongezeka kwa wasiwasi kati ya wachezaji nyota wa mchezo huo. Huku mji wa New York ukiwa umeathiriwa zaidi kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, Shirikisho la Mpira wa Tennis la Marekani limekuwa likijitahidi kutunga mpango utakaoruhusu mashindano hayo kufanyika. Lakini kutokana na Mashindano ya Wazi ya Ufaransa kuahirishwa mpaka Septemba 20, kufutwa kwa mashindano ya Wimbledon na msimu wa mashindano ya tennis kufungwa, kuna wasiwasi zaidi wa kufanyika kwa mashindano ya US Open kwani tarehe iliyopangwa kuanza imekaribia na hali ya maambukizi ya virusi vya Corona bado ni tete. Mashindano hayo yalipangwa kuanza Agosti 31.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako