• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 76,499 wafanyiwa vipimo vya COVID-19 mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2020-06-15 17:12:06

    Msemaji wa kamati ya afya ya manispaa ya Beijing, China, Gao Xiaojun amesema, watu 76,499 wamefanyiwa vipimo vya virusi vya Corona, ambapo watu 59 walikutwa na maambukizi ya virusi hivyo.

    Amesema mpaka kufikia leo asubuhi, vituo 193 vya kufanyia vipimo viliwekwa katika mji wa Beijing ili kuwezesha kufanyika kwa vipimo zaidi.

    Katika wilaya ya Fengtai iliyoko kusini magharibi mwa Beijing, watu 8,950 kutoka Xinfadi, soko kubwa la matunda, mbogamboga na nyama, walifanyiwa vipimo. Ameongeza kuwa, kesi nyingi mpya za maambukizi ya ndani mjini Beijing zinahusiana na soko hilo ambalo kwa sasa limefungwa.

    Wakati huohuo, maofisa wawili mjini Beijing wamefukuzwa kazi baada ya mji huo kuripoti maambukizi ya ndani ya virusi vya Corona.

    Mamlaka za manispaa ya Beijing zimesema, naibu mkuu wa serikali ya wilaya ya Fengtai Zhou Yuqing na Katibu wa Chama wa eneo la Huaxiang katika wilaya hiyo, Wang Hua, wameondolewa kwenye nafasi zao kwa kutotimiza wajibu wa katika ofizi zao wakati wa kazi za kudhibiti na kuzuia kuenea kwa maambukizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako