• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya afya yatahadharisha kuwa mtu aliye a corona bila dalili anaweza kuambukiza wengine

    (GMT+08:00) 2020-06-16 09:04:51
    Wizara ya afya nchini Kenya imetahadharisha kuwa mtu aliye na virusi vya corona lakini hana dalili bado anaweza kuambukiza wengine.

    Aidha serikali imetoa mwongozo wa kujitenga nyumbani kwa wale wanaotaka kufanya hivyo.

    Nchini Kenya kwa sasa walithibitishwa kuwa na virusi vya corona ni 3,727, waliopona ni 1,286 na waliofariki ni 104.

    Wanaopona na wale wanaoondoka karantini wanaruhusiwa kwenda nyumbani.

    Hii iinakuwa ni afueni kwa taasisi za afya ambazo sasa serikali imeonyea kuwa zinafurika.

    Shirika la afya duniani lilikuwa limetangza kuwa kuna watu ambao wameambukizwa virusi vya corona lakini hawana dalili na hawawezi kuambukiza wengine.

    Lakini baadaye limeondoa tangazo hilo kuashiria kuwa bado kuna hatari.

    Na sasa nchini Kenya wizara ya afya inawataka watu wote kujikinga.

    Mkurungezi wa afya ya umma Daktari Francis-Kuria anasema "Awali shirika la afya duniani lilikuwa limetangaza kuwa kuna uwezekano mdogo wa mtu mwenye corona lakini hana dalili, kuambukiza wengine, lakini baadaye ilibainika kwamba sio kweli na sasa tangazo hilo limeondolewa. Bado kuna uwezekano mkubwa kwa mgonjwa kuambukiza wengine hata kama hana dalili. Hivyo kila mtu aendelee kuvaa barakoa"

    Siku chache zilizopita serikali imetangaza mpango wa kujitenga nyumbani ili kupunguza shinikizo kwenye taasisi za afya.

    Lakini sio kila mtu aliye na chumba cha kujitenga, wengine kwenye maeneo ya mijini wanaishi chumba kimoja tu watu 4 au 5.

    Na sasa serikali imesema kujitenga nyumbani, kutafanyika kwa kufuata utaratibu uliowekwa na wizara hiyo na pia utafanyika baada ya kutimiza vigezo vinavyowekwa, Daktari Francis-Kuria anasema, "Tumeweka taratibu za kuwezesha wanaotaka kujitenga nyumbani kufanya hivyo, na ziko kwenye tovuti yetu ya www.health.go.ke . Shirika la afya duniani limeshauri kuwa hakuna haja ya kufanya upimaji wa pili baada ya kutoonyesha dalili zozote baada ya siku 14, lakini bado tunatafiti kuhusu uwezekano wa kupima mara ya pili. Lakini kwa wale ambao wanaodoka karantini baada ya kupimwa na kupatikana bila virusi au dalili bado wanaweza kujitenga wakiwa nyumbani kwao. Lakini kanuni ya kufanya hivyo ni kwamba kuna mtu atayakekuhudumia, mwenye vifaa vya kujikinga. Serikali itatuma mhudumu wa afya kukagua makazi yako na kuruhusiwa kujitenga. Hii itatusaidia kuondoa msongamano kwenye hospitali zetu ambazo hivi karibuni zitajaa".

    Serikali kuu kupitia kwa wizara yake ya afya sasa inapeleka kampeni ya kupambanana na Corona kwenye kaunti.

    Ingawa maeneo mengi ya vijijini kuna karibu asilimia sifuri ya maambukizi, lakini pia iwapo yatatokea maeneo hayo yanakabiliwa na ugumu wa kutoa matibabu kwani bado hakuna vifaa.

    Jumatatu Waziri wa afya Mutahi Kagwe, akiongoza kampeni hiyo kwenye maunti ya Nyandarua anasisitiza umuhimu wa kujitenga, na pia kutokaribisha wageni.

    "Virusi haviwezi kujisambaza vyenyewe, vinasambazwa na watu, ukiona watu wageni kwenye eneo lako, waripoti kwenye viongozi wenu wa mpango wa nyumba kumi, kwa Chifu au kwa serikali ya kaunti ili uendee kuishi bila virusi vya corona. Kupambana na janga la corona sio tu kazi ya serikali pekee lakini pia na watu binafsi ni wajibu wetu sisi wote."

    Kufikia Jumatatu jumla ya sampuli 180,701 zilikuwa zimepimwa nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako