• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kupaka matope kwa makusudi mabaya hakuwezi kukwamisha urafiki kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2020-06-16 10:35:31

    Hivi sasa, janga la virusi vya Corona linaenea kwa kasi barani Afrika. Kwa mujibu wa takwimu kutoka Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa cha Afrika, hadi kufikia tarehe 14 Juni, nchi 54 barani Afrika zimeripoti watu laki 2.3 waliothibitika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo, na idadi ya vifo imezidi elfu 6.2. Idadi ya watu waliothibitishwa kuwa na virusi vya Corona barani Afrika iliongezeka kwa watu laki 1 kutoka sifuri ndani ya siku 98, na ilichukua muda wa siku 18 tu kwa kiasi hicho kuongezeka kutoka laki 1 hadi laki 2. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres alisema katika taarifa ya sera juu ya "Athari za Janga la Virusi barani Afrika", kuwa janga hilo litazidisha kutokuwepo kwa usawa uliodumu kwa muda mrefu uliopita, na kufanya matatizo ya njaa, utapiamlo na magonjwa yawe hatarini zaidi. Na mamilioni ya watu wanaweza kuangukia katika ufakara."
    China ikiwa mwenzi mkubwa zaidi wa kiuchumi barani Afrika, uhusiano kati yake na Afrika umedumu kwa miaka mingi. Pande hizo mbili zimeunda jumuiya ya maslahi ya pamoja, na kujenga jumuiya yenye mustakbali wa pamoja. Katika wakati mgumu zaidi kwa China wa kupambana na janga hili, zaidi ya viongozi 50 wa nchi za Afrika walitoa salamu za pole na misaada kwa China. Wakati janga hilo lilipoibuka barani Afrika, China ilitoa misaada ya vifaa tiba na kutuma wataalamu wa matibabu barani humo. Tovuti ya Deutsche Welle ya Ujerumani imeripoti kuwa, bara zima la Afrika linafanya juhudi za kuzuia kuenea kwa janga hili, na karibu nchi zote za Afrika zinahitaji msaada kutoka China. Hivi sasa timu za matibabu za China zilizosambaa katika nchi 45 barani Afrika zinatoa huduma za matibabu kwa wenyeji wa huko, kuandaa mafunzo zaidi ya mia nne ya kuzuia maambukizi ya virusi ambayo yamewashirikisha maelfu ya wahudumu wa afya. Waziri mkuu wa Guinea Ikweta Francisco Asue amesifu sana ushirikiano uliopo kati ya China na Afrika katika kupambana na maambukizi ya virusi, akisema "China ni mwenzi anayeaminika wa ushirikiano."
    Kwa kushuhudia urafiki kati ya China na Afrika, na ushirikiano katika kupambana na janga la virusi vya Corona, baadhi ya wanasiasa wa Marekani hawajisikii vizuri. Wamechochea mara kwa mara mizozo katika uhusiano kati ya China na Afrika, kusambaza uvumi wa "mtego wa madeni" wa Afrika, na kupaka matope pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Lakini ukweli ni jibu lenye nguvu. Katika miaka miongo kadhaa iliyopita, China imeisaidia Afrika kujenga barabara kuu zenye umbali wa zaidi ya kilomita elfu 10, reli zenye urefu wa zaidi ya kilomita elfu sita, pamoja na idadi kubwa ya maktaba, shule na hospitali. Miradi isiyo ya miundo mbinu ya China imeiletea Afrika mapato ya dola za kimarekani bilioni 50. Kuhusu suala la madeni ya nchi za Afrika, ripoti zilizotolewa hivi karibuni na kundi la Rhodium la Marekani, Benki ya Dunia na mashirika mengine yote yamesema uwekezaji wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" unaleta athari ndogo tu kwa madeni ya nchi zinazohusika, haswa China na nchi za Afrika ziko kwenye hadhi yenye usawa katika mazungumzo kuhusu madeni, na kuheshimu maoni ya Afrika. Zaidi ya hayo, ili kuongeza misaada kwa Afrika kupambana na janga la virusi vya Corona, na kufufua uchumi wa huko, hivi karibuni China pia imetangaza kuwa, itasimamisha ulipaji wa madeni kwa nchi na sehemu 77 ambazo ziko nyuma kiuchumi, zikiwa na nchi nyingi za Afrika.
    Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amesema, "China na Afrika ni marafiki na ndugu, haiwezekani kubadilisha au kudhuru uhusiano mzuri kati ya pande hizo mbili." Mwaka 2019, thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilizidi dola za kimarekani bilioni 200, na China imekuwa mwenzi mkubwa wa kwanza wa biashara barani Afrika kwa miaka 11 mfululizo. Kama waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alivyosema, juhudi za China katika kufanya ushirikiano na nchi za Afrika zinaenea kila mahali, jambo ambalo haliwezi kufanywa na nchi zinazopaka matope ushirikiano huo. Kuhusu suala hilo, wananchi wa Afrika wametambua vizuri. Tarehe 20 Februari, shirika la habari la Afrika Kusini The Citizen lilitoa makala ya "Tusidanganywe na propaganda ya Marekani ya kuipinga China", ikieleza kuwa mbali na kuipaka matope na kuishambulia China, Marekani haikufanya lolote kuisaidia Afrika, na kutoa wito kwa nchi za Afrika zisidanganywe.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako