• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Sasa tutarajie kuona pambano kati ya Tyson Fury na Mike Tyson

    (GMT+08:00) 2020-06-16 10:43:25

    Matarajio ya Tyson Fury kuzipiga na nguli wa mchezo wa masumbwi ulimwenguni, Mike Tyson ambaye ni mmoja kati ya watu anaovutiwa nao yanaelekea kutimia, hii ni baada ya ofa kufika mikononi mwa promota wake Frank Warren. Siku za karibuni kumekuwa na vipande vya video vinavyosambaa mitandaoni vikimuonyesha mkongwe wa masumbwi Mike Tyson mwenye umri wa miaka 53, akifanya mazoezi kwa juhudi huku mashabiki wakitarajia kumuona tena ulingoni. Tyson amekuwa akihusishwa kupambana na mpinzani wake wa miaka mingi, Evander Holyfield lakini, Fury ameingilia kati na kuonyesha kuwa yupo tayari kwa pambano hilo la hisani dhidi ya 'role model' wake. Hata hivyo, promota huyo amekuwa kinyume na mtazamo huo huku akisisitiza kuwa hatojihusisha na pambano hilo endapo litatokea. Tyson, ambaye anafikisha umri wa miaka 54 mwishoni mwa mwezi huu hajajihusisha na mapambano rasmi tangu mwaka 2005 hivyo, Warren anaamini Fury atamuonea huruma ulingoni na hivyo kupoteza ladha za ngumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako