• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Arsenal ipo tayari kujadili mustakabali wa nyota wake Alexander Lacazette

    (GMT+08:00) 2020-06-17 08:54:02

    Klabu ya Arsenal imesema ipo tayari kukaa chini na nyota wake, Alexander Lacazette na kujadili mustakabali wake ndani ya klabu hiyo. Lacazette alianza msimu huu vibaya jambo ambalo lilipelekea kusugua benchi, huku nafasi yake akipewa dogo, Eddie Nketiah aliyerudi kikosini akitokea Leeds alipokuwa akicheza kwa mkopo. Baada ya kuelezwa kuwa Atletico Madrid inahitaji saini yake, Arsenal imepanga wiki zijazo kukutana na mchezaji huyo na kufanya naye mazungumzo. Arsenal kwa sasa imesema haipo tayari kupoteza nyota wake wawili kwa pamoja wanaounda safu ya ushambuliaji ambao ni Lacazette na Pierre Emerick Aubameyang. Mkataba wa Lacazette unatarajiwa kumalizika mwaka 2022 huku Aubameyang ukimalizika 2021. Imeelezwa kuwa kama Aubameyang ataamua kuondoka, basi Lacazette atasalia kuwa mshambuliaji wa kati. Ripoti zinaeleza kuwa, kama Lacazette atauzwa, basi dau lake litakuwa pauni milioni 60 ambazo zitaifanya klabu hiyo kumpata mchezaji wa Atletico Madrid, Thomas Partey.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako