Kwa mujibu wa msomi na mdhadhiri Bwana Omondi Osano, juhudi hizi zitafaulu. Kuhusu mchango na ushirikiano wa China katika kutafuta chanjo na tiba ya virusi vya corona, bwana Omondi anasema kwamba China iko kwenye mstari wa mbele katika juhudi hizi. Hili linadhihirika wazi kutokana na mchango wake kwa Shirika la Afya Duniani (WHO), licha ya kupigwa vita na baadhi ya mataifa.
Vile vile, China inasema kwamba endapo chanjo itapatikana, basi itashirikiana na ulimwengu wote kuhakikisha kwamba kila taifa linanufaika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |