• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Bayern Munich washinda taji lao la 8 mfululizo Bundesliga

    (GMT+08:00) 2020-06-17 16:13:33

    Ushindi mnono wa Bayern Munich wa bao 1-0 dhidi ya Werder Bremen jana usiku, umeiwezesha timu hiyo kutwaa taji lao la nane Bundesliga. Bao la dakika ya 43 la Robert Lewandowski ndilo lilileta tofauti na kumshuhudia Alphonso Davies akilishwa kadi nyekundu kipindi cha pili. Wakiwa na tofauti ya pointi saba mbele ya mahasimu wao wa jadi Borussia Dortmund ikiwa imesalia mechi tatu, Bayern ilihitaji ushindi mmoja tu kutawazwa mabingwa. Ushindi dhidi ya Bremen uliongeza pengo la uongozi wao kwa pointi 76 ambalo ni kubwa kwa Dortmund kuwafikia. Klabu hiyo bado haijapoteza mechi yoyote tangu kurejea kwa Bundesliga, huku ikishinda mechi zote saba iliyoshirki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako