• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Botswana atoa wito wa ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-17 19:45:19

    Rais Mokgweetsi Masisi wa Botswana amesema janga la virusi vya Corona limeonyesha kina cha maingiliano na kutegemeana kwa jamii ya kimataifa.

    Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Viongozi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa uliofanyika kwa njia ya video, rais Masisi amesema ni wazi kuwa kuna haja ya kushirikiana kwa pamoja kama jamii ya kimataifa, serikali, sekta binafsi na taasisi za kijamii kupitia uhusiano wa kivumbuzi.

    Amesema ni wazi kuwa kuna haja ya kufanya kazi kwa pamoja kama jamii ya kimataifa ili kukabiliana kwa ufanisi na janga la virusi vya Corona kwa sababu hakuna nchi inayoweza kufanikiwa peke yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako