• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Beijing yapambana kudhibiti maambukizi ya ndani ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-17 19:54:33

    Mji wa Beijing umeongeza ngazi ya dharura ya kukabiliana na virusi vya Corona kufikia ngazi ya pili kutoka ngazi ya tatu, ikiwa ni ya juu zaidi katika mfumo huo wa ngazi nne, wakati mji huo ukipambana kudhibiti maambukizi mapya ya virusi hivyo.

    Kuanzia tarehe 11 hadi 16 mwezi huu, Beijing imeripoti kesi 137 za maambukizi ya ndani ya virusi vya Corona, na zote zinahusiana na soko la jumla la bidhaa za kilimo la Xinfadi wilayani Fengtai ambalo kwa sasa limefungwa.

    Mkutano wa uongozi wa Chama cha Kikomunisti katika mji wa Beijing imesisitiza kuchukua hatua kali, za uhakika, na zinazofaa, pia kukimbizana na wakati kufanya uchunguzi, vipimo, uchunguzi wa virusi na kutafuta chanzo ili kufunga njia zote za maambukizi ya virusi na kudhibiti hali hiyo haraka.

    Kutokana na kuongezwa kwa ngazi ya hali ya tahadhari, maeneo mengi ya makazi yamefungwa tena mjini Beijing na wale wanaotaka kuingia kwenye maeneo hayo wanapaswa kufuata hatua zilizotolewa.

    Maambukizi hayo mapya yametokea mjini Beijing baada ya China kupata mafanikio ya kimkakati katika kudhibiti janga la virusi vya Corona, na ikiwa kwenye tahadhari dhidi ya kutokea tena mlipuko wa ndani na hata kuingia kwa virusi kutoka nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako