• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona barani Afrika yazidi laki 2.5

    (GMT+08:00) 2020-06-17 20:05:58

    Takwimu zilizotolewa na Kituo cha Kuinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika tarehe 16 zimeonesha kuwa, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona imefikia 252,544, kati yao watu 6,779 wamefariki, na wengine 114,897 wamepona.

    Nchini Camerron, watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo wamefikia 10,140, na kuwa nchi ya 6 yenye idadi kubwa ya maambukizi barani Afrika.

    Nako nchini Tanzania, Rais John Magufuli wa nchi hiyo jana ametangza kuwa, shule zote zitafunguliwa tarehe 29 mwezi huu, na shughuli za jamii

    zilizositishwa kutokana na maambukizi ya COVID-19 pia zitarejea.

    Mtendaji mkuu wa Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (ECA) Bibi Vera Songwe alisema kuwa, nchi za Afrika zinapaswa kuongeza uwekezaji katika sekta ya sayansi na teknolojia, na zinapaswa kujenga uhusiano na ushirikiano wa kirafiki na kuhimisa uvumbuzi kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako