• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Gunners walimwa 3-0 ugenini

    (GMT+08:00) 2020-06-18 17:15:45

    Matumaini ya Arsenal ya kumaliza miongoni mwa vilabu nne bora ilipata pigo kufuatia ushinde wa 3-0 kwa Man City ugani Etihad. Mechi hiyo iliyochezwa jana usiku, ilikuwa siku ya pili tangu Ligi Kuu kurejea baada ya kusitishwa kwa wiki kadhaa. Huku Man City wakiwa tayari nje ya kinyang'anyiro cha kutwaa taji, Arsenal ndio walikuwa wakikaza kamba ili kujipatia tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa. Hata hivyo, hayo yalitibuka, huku Gunners wakikumbana na majeraha mawili kwa mpigo dakika chache kabla ya mechi hiyo. Granit Xhaka ndiye alikuwa wa kwanza kuondoka uwanjani dakika tano kabla ya mechi kuanza baada ya kupata jeraha la mguu. Nafasi yake ilichukuliwa na Dani Ceballos ambaye alijiunga na David Luiz kutoka kwenye benchi dakika 22 baada ya Pablo Mari kupata jeraha. Matokeo hayo yanawacha Arsenal wakishikilia nafasi ya tisa kwenye jedwali na pointi 40 kutoka kwa mechi 29, pointi nane nje ya Ligi ya Mabingwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako