• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yapongeza mkutano kati ya China na Afrika dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-18 17:32:21

    Mkutano maalumu wa kilele wa Mshikamano wa China na Afrika dhidi ya COVID-19 umefanyika kwa mafanikio.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema, China na Afrika zimeshikamana na kuongeza ushirikiano katika kukabiliana na virusi vya Corona, hali hii itaimarisha imani ya kimataifa ya kushinda virusi hivyo, na kutoa mfano mpya wa kuigwa kwa ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na virusi hivyo.

    Zhao amesema hivi sasa maambukizi ya virusi vya Corona bado yanaendelea barani Afrika, nchi za bara hilo zinakabiliwa na changamoto mbalimbali, na kuhitaji misaada zaidi. China inaitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua zaidi, na kuzisaidia kihalisi nchi hizo kushinda virusi hivyo na kutimiza maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako