• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Evariste Ndayishimiye aapishwa kuwa rais wa Burundi

    (GMT+08:00) 2020-06-19 08:41:06

    Rais mteule wa Burundi Evariste Ndayishimiye, aliyeshinda kwenye uchaguzi mkuu wa Mei 20, jana Alhamisi aliapishwa kuwa rais wa nchi hiyo katika mji mkuu wa kisiasa Gitega, katikati ya Burundi.

    Bw. Ndayishimiye amekula kiapo mbele ya wananchi wa Burundi katika uwanja wa michezo mjini Gitega, akiapa kuheshimu Katiba ya Nchi na Katiba ya Umoja, iliyopitishwa mwaka 1991 kwa ajili ya kuleta pamoja makabila matatu ya nchi hiyo, yaani wahutu, watutsi na watwa. Rais Ndayishimiye atatumikia ofisi kwa kipindi cha miaka saba katika muhula wake wa kwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako