• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Kenyatta apongeza ushindi wa Kenya katika uchaguzi wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2020-06-19 10:36:50

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amepongeza ushindi wa nchi hiyo katika duru ya pili ya upigaji kura wa uchaguzi wa wajumbe wasio kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

    Rais Kenyatta ametoa taarifa akisema ushindi huo umeonesha hadhi na ushawishi wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa unaendelea kuongezeka siku hadi siku.

    Nchi hiyo imeshinda kiti hicho baada ya kuishinda Djibouti kwa kupata kura 129 dhidi ya 62 kwenye duru ya pili ya upigaji kura.

    Rais Kenyatta pia amesema, Kenya itafanya juhudi kuimarisha na kueleza hadhi ya Afrika katika baraza la usalama na itahimiza ajenda kumi zilizotolewa kwenye kipindi cha kampeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako