• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapanga kupanua soko kwa sangara wa Nile

    (GMT+08:00) 2020-06-19 10:37:43

    Serikali ya Tanzania imesema inapanga kupanua masoko ya kimataifa ya Amerika Kaskazini na Asia ili kuuza sangara wa Nile kutoka ziwa Victoria.

    Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania Bw. Isack Kamwelwe amesema sangara hao hivi sasa wanauzwa katika masoko ya Ulaya ikiwemo Ubelgiji, Uholanzi, Ujerumani, Ufaransa na Ureno.

    Amesema tangu Mei 20 shirika la ndege la Ethiopia lilipoanza kusafirisha samaki katika masoko ya Ulaya, jumla ya tani 147 za samaki zimesafirishwa katika masoko hayo.

    Bw. Kamwelwe amesema hayo katika mkutano uliowakutanisha mawaziri wa fedha na mipango, mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, mifugo na uvuvi, kilimo, na ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, ambao ulijadili jinsi ya kupanua soko la samaki wa Nile kutoka ziwa Victoria katika maeneo ya Amerika Kaskazini na Asia.

    Ameongeza kuwa mkutano huo umekubali kuyaalika mashirika mengi zaidi ya ndege kote duniani kusafirisha samaki na bidhaa nyingine ikiwemo matunda na mboga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako