• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jukwaa la Vifaa vya Matibabu la Afrika lazinduliwa kukabiliana na uhaba wa vifaa vya kinga dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-19 17:46:55

    Umoja wa Afrika (AU) umezindua Jukwaa la VIfaa vya Matibabu la Afrika linalolenga kukabiliana na uhaba wa vifaa katika vita ya bara hilo dhidi ya mlipuko wa virusi vya Corona.

    Mwenyekiti wa zamu wa Umoja huyo ambaye pia ni rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema, kupitia jukwaa hilo Umoja huo utaweza kukabiliana na uhaba na usalama wa vifaa, kuhakikisha ushindani wa bei na uwazi katika manunuzi, kupunguza ucheleweshaji wa bidhaa, na kutoa jukwaa la pamoja ambapo serikali zinaweza kupata huduma kutoka kwa wasambazaji wenye ubora wa juu na wa kuaminika.

    Amesema jukwaa hilo limeunda kama lango la mtandao wa internet la bara hilo ili kuwezesha kila nchi ya Afrika inaweza kupata vifaa muhimu vya matibabu vinavyohitajika katika kukabiliana na virusi vya Corona.

    Ameongeza kuwa, kwa kupitia jukwaa hilo, nchi za Afrika zinaweza msingi mwingine katika kuendeleza Eneo la Biashara Huria la Afrika, ambalo uzinduzi wake umecheleweshwa kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako