• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Gor Mahia na AFC Leopards wapata mfadhili mpya

    (GMT+08:00) 2020-06-19 21:03:08

    Mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia na AFC Leopards wameingia katika mkataba mpya na kampuni ya mchezo wa bahati nasibu Bet High Kenya, chini ya chapa yao ya BetSafe. Bet High, ambao bado hawajafungua biashara zao nchini, watafadhili vilabu hivyo kwa miaka mitatu. Katika mkataba huo mpya, Gor itakuwa ikipokea kitita cha KSh55 milioni kila msimu huku Leopards wakitia kibindoni KSh40 milioni. Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier, alisema kuwa wana furaha kwa ufadhili huo ambao utawapa usalama na kuwatia nguvu ya kuibuka klabu bora nchini humo. Hii ni mara ya pili kwa vilabu hivyo kufadhiliwa na kampuni moja baada ya mkataba wao na SportPesa ambayo ilifunga biashara zake nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako