• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaandikisha idadi kubwa zaidi ya visa vya Corona,260

    (GMT+08:00) 2020-06-22 06:55:25

    Zimepita siku 100 tangu maambukizi ya virusi vya Corona yaliporipotiwa nchini Kenya.

    Jana katika siku hiyo ya 100,Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alithibitisha idadi kubwa zaidi ya watu 260 waliopatikana na virusi vya Corona ndani ya masaa 24,na kufikisha jumla ya idadi ya watu 4,738 walioambukizwa Corona nchini Kenya kufikia jana.

    Mwnahabari wetu Khamis Darwesh ametuandalia ripoti ifuatayo.

    "Hii safari ni kuanza inaanza sio kuisha inaisha.Hii ni siku ya 100 tu lakini zile zinazokuja ndio nyingi zaidi.Hauendi chini,unaenea zaidi,kwa hivyo na sisi pia ni lazima tujikinge zaidi"

    Wakati akizungumza na wanahabari jana katika jumba la Afya jijini Nairobi,Waziri wa Afya nchini Kenya,Mutahi Kagwe alisema kati ya visa 260 vilivyothibitishwa jana ,254 kati yao ni wakenya ilhali wengine sita ni raia wa kigeni.

    Waziri Kagwe alisema vipimo vimekuwa vikiongezeka kila mwezi tangu kisa cha kwanza cha Corona kiliporipotiwa nchini.

    "Madaktari wetu sasa wamekuwa wataalamu maalum,wanaelewa ni kitu gani tunafanya.Wanatusaidia sana.Tulikuwa hata hatuna reagents za kupima watu kama wana Corona ,tumepata hizo.Tulikuwa hatuna vitanda vya kupeleka watu watu wakipata huu ugonjwa,sasa tunaelewa.Ilikuwa ugonjwa wenyewe hatuuelewi"

    Waziri Kagwe alisema licha ya changamoto zilizojitokeza siku za kwanza,sasa hivi Kenya imejifunza na inaelewa mengi kuhusu ugonjwa wa maambukizi ya virusi vya Corona,na pia inaendelea kupiga hatua kubwa katika kuudhibiti.

    "Hii safari ilipoanza kusema kweli tulikuwa hatuelewi mambo ya virusi vya Corona.Tulitoka pahali ambapo kulikuwa kugumu sana.Tuliona mambo ambayo yalikuwa ya ajabu,tulisikia mambo ambayo hatuelewi lakini siku hizi tushajifunza kidogo"

    Aidha Kagwe alisema Wizara ya Afya imewaruhusu wagonjwa 550 wa corona wasioonyesha dalili zozote kutoka hospitali kwa ajili ya kupata uangalizi wakiwa nyumbani baada ya kukamilisha karantini ya lazima ya siku 14 katika vituo mbalimbali vya kujitenga nchini.

    Hospitali ya rufaa ya Chuo Kikuu cha Kenyatta imewaruhusu wagonjwa 338 kwenda kupata uangalizi nyumbani ilhali hospitali Kuu ya Mkoa wa Pwani mjini Mombasa iliwaruhusu wagonjwa 212.

    Uamuzi wa kuwaruhusu wagonjwa ambao sio mahututi ulifikiwa baada ya kuongezeka kwa visa vya Corona katika hospitali mbalimbali huku hospitali ya Mbagathi jijini Nairobi na hospitali ya Rufaa ya Chuo Kikuu cha Kenyatta zikikaribia kujaa wagonjwa wa Covid-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako