• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yathamini juhudi za China kuhimiza ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-22 08:38:22

    Waziri wa mambo ya nje wa Misri Bw. Sameh Shoukry jana usiku alisema Misri inathamini juhudi za China kuhimiza ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na janga la COVID-19.

    Bw. Shoukry amesema hayo alipokutana na balozi wa China nchini Misri Bw. Liao Liqiang huko Cairo, ambapo maofisa hao wawili walijadili uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili. Bw. Shoukry amesema uzoefu wa mafanikio ya China katika mapambano dhidi ya janga la COVID 19 unastahili kuigwa na nchi zote, na Misri iko tayari kushirikiana na China kuzidisha uhusiano na ushirikiano kati ya Afrika na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako