• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Liverpool kufanya usajili wa kibabe

    (GMT+08:00) 2020-06-22 15:55:26

    Klabu ya Liverpool imepanga kumsajili nyota wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe kwa kubadilishana na mchezaji wao, Sadio Mane na kitita cha paundi milioni 200. Kama usajili huo utafanikiwa utaandika historia nyingine kwenye mchezo wa soka baada ile ya Neymar kutoka Barcelona mwezi Agosti mwaka 2017 na kujiunga na PSG kwa dau nono kama hilo. Mabosi wa Liverpool wana wasiwasi na mustakabali wa Sadio Mane, ambaye mpaka sasa bado hajakubali kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kusalia Anfield. Liverpool wamejipanga kuhakikisha wanafanya usajili mkubwa kunako dirisha lijalo la usajili, huku wakiwa hawana uhakika wa kumbakiza nyota wao Mane. Sadio Mane amekuwa katika wakati mzuri msimu huu, akiwa tayari na jumla ya magoli 14 akichangia pasi za mwisho tisa (9) zilizozalisha magoli kwenye michezo yake 26 ya Premier League.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako