• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 22 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya wafanyika

    (GMT+08:00) 2020-06-22 18:41:24

    Mkutano wa 22 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya umefanyika leo kwa njia ya video, na kuhudhuriwa na rais Xi Jinping wa China, mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Charles Michel na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.

    Huu ni mkutano wa kwanza kati ya viongozi wa China na viongozi wa awamu mpya wa Umoja wa Ulaya, pia ni mawasiliano ya ngazi ya juu zaidi kati ya China na Ulaya baada ya kutokea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang, Bw. Michel na Bi. von der Leyen wameendesha mkutano huo kwa njia ya video. Viongozi wa pande hizo mbili wamesisitiza kuwa watajitahidi kuhimiza makubaliano ya uwekezaji kati ya China na Ulaya kufikiwa ndani ya mwaka huu, pia wamekubaliana kuongeza juhudi kubwa zaidi kufikia makubaliano ya utaratibu kuhusu ushindani wa haki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako