• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wiki ya biashara kati ya China na Afrika kufanyika kwa njia ya mtandao mwishoni mwa wiki hii

    (GMT+08:00) 2020-06-23 09:02:27

    Wiki ya biashara kati ya China na Afrika inatarajiwa kufanyika kati ya Juni 29 na Julai 5, ili kuonyesha maendeleo ya uhusiano wa kibiashara kati ya China na Afrika, licha ya kuwepo changamoto kutokana na virusi vya Corona.

    Kampuni inayoandaa maonyesho hayo MIE imesema maofisa wa serikali, wawekezaji na waonyesha bidhaa kutoka China na Afrika watashiriki kwenye maonyesho hayo ya wiki moja yatakayofanyika kwa njia ya mtandao. Kampuni hiyo imesema jukwaa la maonyesho kwa njia ya mtandao la "Global Trade week" litashirikisha waonyesha bidhaa 1,000.

    Maofisa waandamizi wa China na Afrika ambao wamethibitisha kushiriki kwenye maonyesho hayo, wanatarajiwa kutoa hotuba kwenye ufunguzi, na kurejea ahadi zao za kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya pande mbili.

    Waandaaji pia wamesema kila siku kutakuwa na fursa ya kuonyesha fursa za uwekezaji kutoka nchi za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako