• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uanachama usio wa kudumu wa Kenya kwenye UM utasaidia kutatua mizozo, mapigano na kuleta amani (Ronald Mutie)

    (GMT+08:00) 2020-06-23 09:57:21

    Uanachama usio wa kudumu wa Kenya kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unatasaidia sio tu nchi hiyo lakini bara lote kuendelea kutatua mizozo, mapigano na kuleta amani katika nchi zilizoathrika.

    Mtaalam wa maswala ya usalama nchini Kenya Bwana Mwenda Mbijiwe amesema uanachama huo pia utawezesha nchi hiyo kushiriki katika maamuzi yanayohusu maazimio ya Umoja wa Mataifa katika maswala ya amani na usalama.

    Amesema tayari Kenya inashiriki kwenye oparesheni ya kuleta amani kwa kutuma wanajeshi wake nchini Somalia kujiunga kwenye kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika AMISOM akitaja ushiriki huo kama uzoefu muhimu.

    Lakini kwingineko barani Afrika, nchi kama vile Nigeria bado zinakabiliwa na mashambulizi ya kundi la Boko Haram, nayo Sudan kusini inazongwa na vita vya ndani.

    Hivyo Mwenda anasema Kenya itakuwa na jukumu kubwa kuwakilisha maslahi ya nchi hizo kwenye meza ya Umoja wa Mataifa.

    Baadhi ya maslahi hayo ni kama kushawishi Umoja wa Mataifa kutenga fedha zaidi kwa nchi husika ili kuzisaidia kuboresha uwezo wao wa kijeshi na kuimarisha usalama wa ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako