• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yatoa redio bila malipo kusaidia wanafunzi kujisomea majumbani wakati wa mlipuko wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-23 16:45:34

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema, serikali yake itatoa redio bila malipo kusaidia wanafunzi kujisomea majumbani wakati huu wa mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

    Rais Museveni amesema, wataanzisha mpango wa elimu kwa kupitia vipindi vya radio, na kwamba ingawa alipendelea zaidi kutumia TV, lakini wanasayansi wamesema, TV italeta mkusanyiko wa watu vijijini.

    Rais Museveni pia amesema, machapisho ya vitabu vya elimu pia yatatolewa kusaidia wanafunzi kujifunza wakiwa nyumbani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako