• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wamarekani wenye asili ya Afrika wako hatarini zaidi kulazwa hospitali kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-23 17:02:09

    Wamarekani wenye asili ya Afrika wenye bima ya afya nchini Marekani wako hatarini zaidi kulazwa hospitali kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona kuliko Wamarekani weupe.

    Takwimu hizo zilizotolewa na Vituo vya Bima ya Afya na Huduma za Afya (CMS) zimeonyesha kuwa, Wamarekani wenye asili ya Afrika waliolazwa kutokana na virusi vya Corona wamefikia 465 kati ya wagonjwa laki moja, ikiwa ni mara nne zaidi ya kiwango cha wazungu, ambacho ni 123 kwa wagonjwa laki moja.

    Zaidi ya watu 325,000 waliokuwa kwenye mfumo wa bima ya afya waligunduliwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona kati ya Januari Mosi na Mei 16, na watu 110,000 wenye bima hiyo walilazwa kutokana na maambukizi hayo katika kipindi hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako