• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema India inapaswa kuwajibika na mapambano kati ya pande hizo mbili kwenye sehemu ya mipakani

    (GMT+08:00) 2020-06-24 16:53:36

    Mkurugenzi wa Idara ya habari kwenye Wizara ya Ulinzi ya China Bw. Wu Qian amesema, India inapaswa kuwajibika na mapambano kati ya majeshi ya nchi hizo kwenye sehemu ya Bonde la Gallevan.

    Amesema China inaitaka India kuwaadhibu vikali walioanzisha mapambano, na kudhibiti kwa makini majeshi yake ili kuepusha tukio kama hilo lisitokee tena.

    Bw. Wu Qian amesema, China ina mamlaka kamili juu ya Bonde hilo, na jeshi la China limekuwa ikifanya doria kwenye eneo hilo. Tokea mwezi Aprili, jeshi la India lilianza kujenga kambi kwenye sehemu ya mipaka ya eneo hilo, hatua ambayo imepingwa mara nyingi na China. Usiku wa tarehe 15, jeshi la India lilivuka mpaka, na kuwashambulia wanajeshi wa China, hatua iliyosababisha mapambano makali kati ya wanajeshi wa pande zote mbili, na kusababisha vifo na majeruhi.

    Bw. Wu amesisitiza kuwa baada ya tukio hilo, mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo mbili wamefanya majadiliano kwa njia ya simu, na walipanga kufanya mazungumzo ya pili ya ngazi ya kapteni tarehe 22 Juni, ili kubadilishana maoni kuhusu kudhibiti hali ya wasiwasi, na kulinda amani na utulivu kwenye sehemu ya mipaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako