• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maambukizi ya COVID-19 yanayohusiana moja kwa moja na Soko la Xinfadi mjini Beijing yadhibitiwa

    (GMT+08:00) 2020-06-25 08:34:06

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana alasiri, msemaji wa serikali ya mji wa Beijing Bw. Xu Hejian amesema, hali ya maambukizi ya COVID-19 inayohusiana moja kwa moja na soko la jumla la kilimo la Xinfadi imedhibitiwa kimsingi, lakini wakati huo huo maambukizi kutokana na mikusanyiko ya kifamilia na kwenye sehemu za kazi, na maambukizi mitaani yametokea, hali ya kinga na udhibiti wa ugonjwa huo bado ni tete.

    Kwenye mkutano huo mkurugenzi wa kamati ya afya ya Beijing Bw. Lei Haichao, amesema kati ya wagonjwa 256 waliothibitishwa mjini Beijing, watu 253, ambao ni asilimia 98.8, wanahusiana moja kwa moja na soko la Xinfadi, na wengine watatu bado wanahitaji kuchunguzwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako