• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa WHO wasema mlipuko wa COVID-19 haujafikia kileleni katika mabara ya Amerika

    (GMT+08:00) 2020-06-25 08:36:02

    Mkurugenzi mtendaji wa Mipango ya Dharura wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Michael Ryan amesema mlipuko wa virusi vya Corona bado haujafikia kileleni katika mabara ya Amerika, ambayo yanatarajiwa kushuhudia vifo zaidi katika wiki kadhaa zijazo.

    Bw. Ryan amesema hali ya maambukizi ya COVID-19 katika mabara ya Amerika ni mbaya kwa ujumla, hasa katika Amerika ya Kati na Kusini, ambako nchi nyingi zimeshuhudia ongezeko la asilimia 25 hadi 50 la maambukizi katika wiki iliyopita. Wakati huohuo, Katibu mkuu wa WHO Bw. Tedros Ghebreyesus amesema idadi ya maambukizi ya COVID-19 kote duniani inatarajiwa kufikia milioni 10 ndani ya wiki ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako