• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Trump asema "huenda" atatuma vikosi vya Marekani kutoka Ujerumani kwenda Poland

    (GMT+08:00) 2020-06-25 08:36:47

    Rais Donald Trump wa Marekani jana jumatano amesema huenda atatuma vikosi vya Marekani kutoka Ujerumani kwenda Poland.

    Rais Trump amesema hayo kwenye mkutano na wanahabari akiambatana na mwenzake wa Poland Andrzej Duda ambaye yuko ziarani nchini Marekani.

    Rais Duda ambaye ni kiongozi wa kwanza wa nchi ya nje kufanya ziara nchini Marekani tangu virusi vya Corona vilipuke, pia amesema kuna uwezekano wa kuongezwa zaidi kwa vikosi vya Marekani nchini Poland.

    Hatua hiyo inaweza kuongeza wasiwasi wa Russia, ambayo imesisitiza mara nyingi kupinga uwepo wa kijeshi wa NATO karibu na mpaka wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako