• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yasisitiza mwito wa kufutwa madeni wakati wa mapambano dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-25 08:55:23

    Serikali ya Tanzania imesisitiza mwito wake kwa wakopeshaji kufuta madeni kwa nchi zinazoendelea ili kuzisaidia nchi hizo kupambana na virusi vya Corona.

    Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Bw. Palamagamba Kabudi amesema kufutwa kwa madeni kutaziwezesha nchi zinazoendelea, ikiwa ni pamoja na Tanzania, kutumia fedha zilizotakiwa kulipia madeni kupunguza madhara ya virusi vya Corona.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, imesema waziri Kabudi ametoa mwito huo kwenye mkutano kwa njia ya video na nchi za jumuiya ya madola.

    Taarifa pia imesema mkutano huo umejadili jinsi mashirika ya kimataifa yanavyoweza kuziunga mkono nchi zinazoendelea kujenga uwezo wa kutengeneza vifaa tiba na kuziwezesha kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako