• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la IMF lakadiria kuwa uchumi wa dunia utashuka kwa asilimia 4.9 mwaka huu

    (GMT+08:00) 2020-06-25 09:15:28

    Shirika la fedha la kimataifa IMF limetangaza ripoti ya mustakabali wa uchumi wa dunia ikikadiria kuwa uchumi wa dunia kwa mwaka 2020 utaporomoka kwa asilimia 4.9.

    Ripoti hiyo imesema athari hasi za kiuchumi zinazotokana na janga la virusi vya Corona na hatua za kudhibiti na kuzuia kuenea kwa virusi hivyo zimezidi makadirio ya awali, hasa zimeathiri zaidi familia zenye kipato cha chini. Pia mchakato wa kufufua uchumi wa dunia unaendelea polepole kuliko ilivyokadiriwa. Kutokana na kuendelea kutekelezwa kwa hatua mbalimbali dhidi ya COVID-19 katika nusu ya pili ya mwaka huu, shirika hilo limekadiria kuwa mwaka huu uchumi wa dunia utashuka kwa asilimia 4.9 lakini mwaka kesho unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako